Mlipuko mbaya zaidi wa kipindupindu nchini Malawi katika miongo kadhaa umesababisha mahitaji makubwa ya chanjo lakini hifadhi inaripotiwa kupungua.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, vilimnukuu Msemaji wa Wizara ya Afya ya Malawi, Adrian Chikumbe akisema nchi hiyo haina chanjo zaidi ya kipindupindu.
Wilaya 29 za Malawi ziliripoti matukio ya kipindupindu tangu kuthibitishwa kwa kesi ya kwanza Machi 2022, ambapo Mamlaka za Afya za Malawi ziliripoti jumla ya visa vipya 631 vya kipindupindu na vifo 17.
Katika sasisho lake la kila siku, Wizara ya Afya nchini humo iliwataka Wamalawi wote kuzingatia hatua za kuzuia na kudhibiti ugonjwa huo.
Kipindupindu, ni ugonjwa wa kuharisha unaoenezwa kupitia maji na vyakula vichafu, ambavyo vinaweza kusababisha upungufu mkubwa wa maji mwilini.