Waandishi wa Habari nchini Tunisia wameungana na Wanaharakati wa haki katika maandamano yaliyofanyika katika mitaa ya mji mkuu wa Tunis, kushutumu ukandamizaji wa Serikali na majaribio ya kuvitishia vyombo vya habari.

Maandamano hayo, yaliyoandaliwa na chama cha wanahabari, SNJT, yamekuja ikiwa ni siku tatu baada ya Polisi kumkamata Mkurugenzi wa kituo maarufu cha redio cha kibinafsi, Mosaïque FM, Noureddine Boutar.

Waandishi wa habari wa Tunisia walipokuwa katika maandamano ya kudai uhuru wa vyombo vya habari nje ya Jumuiya ya Kitaifa ya Wanahabari wa Tunisia (SNJT). Picha ya Fethi Belaid/AFP.

Boutar anafanya idadi watu waliokamatwa tangu Februari 11, 2023 kufikia 10, wengi wakiwa ni wakosoaji wa Rais wa nchi hiyo Kais Saied, wakiwemo wanachama wa chama chenye msukumo wa Kiislamu cha Ennahdha.

Makamu wa rais wa chama cha waandishi wa habari – SNJT, Amira Mohamed anasema “Mamlaka, katika ngazi zote ikiwa ni pamoja na rais na waziri mkuu, wanakandamiza uhuru wa vyombo vya Habari madai ambayo Rais Kais Saied anayakanusha.

Mchengerwa azindua magari 22 ya doria TAWA, ataka kazi
Habari Picha: Rais Samia uwanjani Bole mkutano AU