Jeshi la Polisi nchini Somalia limesema takriban watu watano wameuawa na wengine 11 kujeruhiwa, akiwemo Gavana Gedo Ahmed Bulle Gared, katika shambulio la kujitoa mhanga lililotokea kusini magharibi mwa nchi hiyo.

Shambulio hilo, japo hakuna kundi lililojitokeza kudai kuhusika lakini linahisiwa kutelekezwa na wanamgambo wa Al Shabab, wenye mfungamano na Al-Qaeda na ambao mara kwa mara hufanya mashambulizi ya kujitoa mhanga katika nchi hiyo isiyo na utulivu.

Sehemu ya uharibifu unaodaiwa kusababisha vifo vya watu watano na majeruhi 11. Picha ya DW.

“Mlipuaji wa kujitoa mhanga aliendesha gari lililokuwa na vilipuzi kwenye nyumba ya wageni huko Bardera ambako maafisa wa serikali walikuwa wakiishi,” amesema Kamanda wa Polisi wa mji wa mkoa wa Gedo, Hussein Adan uopo kilomita 450 mashariki mwa mji mkuu Mogadishu.

Mbali na kifo cha Gavana huyo, pia makamanda kadhaa wa kijeshi waliuawa na mlipuko huo uliharibu sehemu kubwa ya jengo na maafisa watano wa usalama pia wameuawa, huku Adan akibainisha hayo bila kutoa maelezo zaidi kuhusu ukubwa wa tatizo.

Vigogo Young Africans watenga mzigo mzito
Waziri Mkuu ataka sheria bora usalama barabarani