Mabosi klabu ya Young Africans wanaangalia uwezekano wa kuwaongezea Bonasi wachezaji wao ili walipe kisasi cha kuwafunga wapinzani wao US Monastir ya nchini Tunisia.

Young Africans itakuwa mwenyeji wa mchezo huo wa Mzunguuko watano wa Kundi D, Kombe la Shirikisho Barani Afrika Jumapili (Machi 19) kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo wao wa kwanza uliopigwa huko Tunisía, Young Africans ilifungwa bao 2-0.

Taarifa kutoka ndani ya Benchi la Ufundi la klabu hiyo, zimeeleza kuwa Uongozi wa juu unaupa umuhimu mkubwa mchezo huo ambao wataingia uwanjani kupambana kufa au kupona.

Mtoa taarifa hizo amesema kuwa, katika kuhakikisha morali ya wachezaji inaongezeka, uongozi umepanga huo ambao muhimu kupata ushindi ili kujiweke katika nafasi nzuri ya kufuzu Robo Fainali.

“Ile ari ya wachezaji uliyoiona katika mchezo wa ligi dhidi ya Geita Gold itaongezeka kwa kiasi kikubwa tutakapocheza katika mchezo wa kimataifa dhidi ya US Monastir,”

“Kwa kifupi uongozi hautaki kupoteza mchezo huu ambao utawapa picha kamili ya safari yao kufuzu Robo Fainali kabla ya kwenda kurudiana dhidi ya TP Mazembe nyumbani kwao,” amesema mtoa taarifa huyo

Rais wa Young Africans, Injinia Hersi Said mwanzoni mwa juma hili alizungumzia hilo la Bonasi kwa kusema: “Kila mchezo tunaoucheza wa ligi au kimataifa inakuwepo Bonasi kwa upande wa timu ambayo ipo katika mikataba ya wachezaji wetu ambayo ni siri.

“Pia zipo Bonasi kutoka kwa baadhi ya wadau wanaotoa hamasa na morali ya wachezaji kwa kutoa ahadi zao kutokana na umuhimu wa mchezo hasa kimataifa, kama ilivyokuwa kwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan aliyetoa ahadi nunua kila bao kwa Sh 5Mil.”

Mchengerwa azindua Boti ya Kitalii TAWA Sea Cruiser
Wanne wauawa kwa shambulio la bomu akiwemo Gavana