Ikiwa ni siku chache baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu – ICC kutaka Rais wa Urusi, Vladimir Putin akamatwe kwa makosa ya uhalifu wa kivita, Kiongozi huyo aliwasili Crimea kwa ziara ya kushtukiza ya kuadhimisha mwaka wa tisa wa Urusi kunyakua peninsula hiyo ya Ukraine.

Akiwa eneo hilo, Putin alipokelewa na gavana wa Sevastopol, Raz Razvozhayev aliyewekwa rasmi na Urusi, Mikhail Razvozhayev, na alipelekwa kuona kituo kipya cha watoto na shule ya sanaa juu ya kile afisa huyo alisema kuwa ni ziara ya ghafla huku kukiwa na maoni tofauti juu ya ziara hiyo.

Kikundi cha waendesha Pikipiki wa Urusi ‘Nochniye Volki’ (The Night Wolves), wakiwa na bendera za Taifa la Urusi kuelekea Sevastopol wakihudhuria mkutano wa magari wa kuadhimisha mwaka wa tisa. Picha ya AP.

Vyombo vya habari vya serikali, havikutangaza matamshi yoyote kutoka kwa Putin siku moja baada ya ICC, kusema kuwa imetoa hati ya kukamatwa kwake na kumshutumu kwa uhalifu wa kivita wa kuwafukuza kinyume cha sheria mamia ya watoto kutoka Ukraine na baadhi ya watu kuhoji uhalali wa kumkamata.

Urusi iliiteka Crimea mwaka 2014, ikiwa ni miaka minane kabla ya kuanza uvamizi wake kamili nchini Ukraine, inayosema itapigana kuiondoa Urusi kutoka Crimea na maeneo mengine yote ambayo Urusi imekalia katika vita vya mwaka mzima.

Maandamano: Ruto asema hataruhusu uchochezi
Mayanga awatuliza mashabiki Mtibwa Sugar