Mahakama ya kimataifa ya uhalifu – ICC, imetoa hati ya kumkamata Rais wa Urusi, Vladimir Putin ikimshtumu kwa muhusika na uhalifu wa kivita nchini Ukraine.

ICC imetoa hati ya kumkamata Putin kwa tuhuma za kuwahamisha kinyume cha sheria watoto na raia wengine wa Ukraine hadi Russia.

Kamishna wa haki za watoto wa Russia, Maria Alekseyevna Lvova-Belova. Picha ndogo ni Rais wa Urusi, Vladmir Putin. Picha ya Newsweek.

Mahakama hiyo, pia imetoa hati ya kumkamata Kamishna wa haki za watoto wa Russia, Maria Alekseyevna Lvova-Belova kutokana na tuhuma hizo zilizotolewa dhidi ya Putin.

Hatua hiyo hata hivyo, imekuwa ikikanushwa na Urusi juu tuhuma kwamba wanajeshi wake kufanya ukatili wakati wa uvamizi wa Russia dhidi ya jirani yake ambao umedumu kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Chanjo yasababisha virusi vya Polio, watoto sita walazwa
Adai kupewa kesi ya ubakaji kwa kumkataa mke wa Bosi