Wizara za afya za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, zimegundua uwepo wa virusi vya polio vinavyotokana na chanjo, baada ya kuthibitishwa kwa visa viwili vya mtoto wa kiume (4), katika wilaya ya Isale magharibi mwa Bujumbura na watoto wengine wawili wa DRC.

Shirika la Afya Duniani – WHO, Mpango wa Kutokomeza Polio Ulimwenguni limesema sampuli nyingine tano kutoka kwa wafuatiliaji wa mazingira ya maji machafu zimethibitisha uwepo wa virusi vya polio vya aina mbili, vinayosambaa nchini Burundi.

Virusi hivyo, ni tofauti na vile ambavyo havitokani na chanjo, vikiwa na maambukizi yanayotokea wakati virusi vya polio vilivyoko katika chanjo ya mdomo vinapodhoofika na kusambaa miongoni mwa watu, ambao hawakupata chanjo kwa muda mrefu.

Oral Polio vaccine (OPV). Picha ya BSIP/Universal Images Group

Mpango wa Kutokomeza Polio Duniani – GPEI, kupitia taarifa yake umeeleza kuwa kusambaa kwa virusi vya polio aina ya 2, vinavyotokana na kinga vimegundulika kwa watoto sita katika majimbo ya Kivu Kusini na Tanganyika, mashariki mwa DRC.

Hata hivyo, Wizara ya Afya nchini Burundi imesema ina mpango wa kufanya kampeni ya chanjo ya polio katika wiki zijazo kwa watoto wote wanaostahiki, walio na umri wa hadi miaka 7 kwa msaada wa WHO na GPEI.

Taarifa ya GPEI imeeleza kuwa, dozi milioni 600 za chanjo hiyo mpya zimetolewa katika nchi 28 tangu mwezi Machi 2021, ambayo inadaiwa kuwa salama na yenye ufanisi huku Wizara ya Afya ya DRC ikipanga kufanya kampeni ya chanjo hiyo mwezi Aprili, 2023.

Wachezaji Simba SC waahidiwa Milioni 250
ICC yatoa hati ya kukamatwa kwa Rais Putin, Maria Belova