Kiongozi wa Upinzani nchini Kenya Raila Odinga, amedai kunusurika katika jaribio la kuuawa wakati wa maandamano ya kuipinga Serikali, baada ya gari lake kupigwa risasi mara kadhaa alipokuwa akiliendesha kuzunguka mji mkuu wa nchi hiyo Nairobi, akiwakusanya waandamanaji.
Raila ameyasema hayo mbele ya Waandishi wa Habari na kuongeza kuwa urushaji huo wa rsasi kulilenga gari lake ulikuwa una nia ya kumuuwa kwani hadhani kama afisa yeyote wa polisi anaweza kulenga kuwapiga risasi wanasiasa bila amri kutoka juu.
Amesema, “Magari mawili ya kunisindikiza pia yalikuwa yamevunjwa vioo vyake vya mbele. Ndani ya magari hayo harufu kali ya mabomu ya machozi bado ilikuwa ipo na nimewaagiza mawakili wangu waende mahakamani kushughulikia tukio hili.”
Mgombea huyo wa muda mrefu wa urais mwenye umri wa miaka 78 amesisitiza kuwa maandamano hayo yatakoma mara baada ya baada ya Serikali kupunguza gharama ya vyakula vya msingi na kuruhusu upatikanaji wa matokeo ya uchaguzi wa 2022 kutoka kwa Vitendea kazi vya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka, IEBC.
Wapinzani nchini Kenya, wanamlaumu Rais William Ruto kwa kupanda kwa gharama ya maisha na unadai alihujumu uchaguzi wake kinyume cha sheria katika uchaguzi wa mwaka jana, ingawa Mahakama ya Juu Zaidi, imeidhinisha uhalali wa matokeo ya uchaguzi huo.
Rais Ruto, ambaye Alhamisi aliwasili nchini kutoka kwa safari ya siku nne nchini Ubelgiji na Ujerumani, amesalia na msimamo kuwa maandamano yanayoendelea yapo kinyume cha sheria huku
Polisi wamekidaiwa kutumia nguvu kuwatawanya waandamanaji, na hadi sasa tayari watu wanne wanaripotiwa kufariki tangu kuanza kwa maandamano hayo wiki iliyopita.
Hata hivyo, Mamlaka huru ya Uangalizi wa Polisi inachunguza matukio manne ya polisi kuwapiga risasi na kuwaua waandamanaji pamoja na madai kwamba polisi walishindwa kujibu ripoti kuhusu uharibifu wa mali binafsi, huku ikiwataka Askari kuzingatia sheria kwa kulinda maisha ya watu na mali.