Rais wa Kenya, William Ruto ameagiza Mchungaji Paul Mackenzie ambaye aliwataka Wafuasi wake kufunga hadi kufa ili waende mbinguni haraka na kupelekea Waumini kupoteza maisha ambapo hadi sasa miili 58 imegunduliwa kufunguliwa mashitaka.

Agizo la Ruto linakuja muda mfupi baada ya Polisi kupata miili mingi zaidi kutoka kwenye kaburi la pamoja karibu na Kijiji kilichopo katika kaunti ya Kilifi ikifikisha idadi ya miili iliyofukuliwa kuwa 58 ambapo maafisa Wakuu wa usalama wakiongozwa na IGP Japhet Koome na Mkuu wa Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mohamed Amin wanatarajiwa kujiunga na Timu ya wachunguzi.

Idadi ya waliofariki imekuwa ikiongezeka kwa kasi huku ufuakuaji wa makaburi hayo ukiendelea ambapo inaarifiwa kuwa idadi inaweza kuongezeka zaidi kwani Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya limesema Watu 112 wamepotea kwenye dawati la ufuatiliaji.

Paul Mackenzie anadaiwa kuwalazimisha Waumini wake kuanzia Watoto wadogo hadi Watu wazima kufunga kula chakula hadi kufa kama njia ya moja kwa moja ya kufika kwa Mbinguni, na anadaiwa kuwa amefanya mgomo wa kula akiwa Mahabusu.

Young Africans yapiga hesabu kali Kwa Mkapa
Mzamiru: Hatuyapi nafasi yanayosemwa, tutapambana