Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule ameongozana na Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Ally Gugu na Mkurugenzi wa Jiji, Joseph Mafuru kupokea ugeni kutoka China ukiongozwa na HuaRong Zhang mmiliki wa Huajian Group Company akiwa na lengo la kuwekeza katika Kiwanda kikubwa cha kutengeza viatu.

Senyamule amemshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufungua fursa za uwekezaji nchi na amewakaribisha wawekezaji hao na kuwahakikishia mazingira rafiki ya uwekezaji katika Mkoa wa Dodoma. Pia amemshukuru Dkt. Tausi Kida Katibu Mkuu uwekezaji na Gilead Teri kwa kumleta mwekezaji huyo wa kimkakati.

Coastal Union yaachana na Emery Nimubona
Kocha Mbeya City matumaini kibao Ligi Kuu