Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amesema katika mwaka wa fedha 2023/24, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi inaomba kuidhinishiwa jumla ya Shilingi 3,554,783,957,000.00.

Prof. Mbarawa amewasema hayo wakati akiwasilisha Bajeti ya Wizara hiyo katika mwaka wa Fedha 2023/2024 na kudai kuwa kati ya fedha hizo, Shilingi 1,468,238,449,000.00 ni kwa ajili ya Sekta ya Ujenzi na Shilingi 2,086,545,508,000.00 ni kwa ajili ya Sekta ya Uchukuzi.

Amesema, “Shilingi 1,468,238,449,000.00 za Fungu 98 (Ujenzi) zinajumuisha Shilingi 48,395,392,000.00 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Shilingi 1,419,843,057,000.00 ni kwa ajili ya Bajeti ya Maendeleo.”

Aidha, Prof. Mbarawa ameongeza kuwa Sekta ya Uchukuzi inaombewa jumla ya Shilingi 2,086,545,508,000.00. Kati ya hizo, Shilingi 118,215,599,000.00 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Shilingi 1,968,329,909,000.00 ni kwa ajlili ya Miradi ya Maendeleo.

Marcus Rashford kusaini mkataba mpya Man Utd
Azam FC kushusha vifaa vya Afrika Magharibi