Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameupongeza Wakala wa Umeme Vijijini – REA, kwa kuendelea kuhakikisha wanaratibu mpango kupeleka umeme vijijini.
Majaliwa ameyasema hayo jijini Dodoma katika viunga vya Bunge, huku akitoa wito kwa Watanzania kubadilika na kutumia nishati mbadala, ili kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi.
Amesema, “Wale mliopewa jukumu la kusimamia hili, jiridhisheni na kuhakikisha kila kijiji kinapata umeme, na muwasimamie wakandarasi ili wafanye kazi hiyo kikamilifu.”
Awali, Waziri wa Nishati, Januari Makamba alisema wizara hiyo nayo tayari imejipanga ifikapo Julai 2023 kuzindua dira ya Nishati Safi ya kupikia na kusisitiza kuwa Juni 2024 kila kijiji nchini kitakuwa na umeme.