Mahakama ya Burundi, imemnyima dhamana Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo, Alain-Guillaume Bunyoni, ambaye ameshtakiwa kwa shutuma za kuhujumu usalama wa Taifa na kumtusi Rais.

Bunyoni ambaye pia alikuwa Mkuu wa Polisi na Waziri wa Usalama wa Ndani, alikuwa akionekana kama Mkuu wa Baraza la Viongozi la Kijeshi linalojulikana kama “Majenerali” wenye nguvu ya kweli ya kisiasa nchini Burundi.

Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo, Alain-Guillaume Bunyoni. Picha ya Tchandrou Nitanga / AFP.

Hata hivyo, alikamatwa Aprili 2023 katika mji Mkuu wa Taifa hilo Bujumbura usiku wa kuamkia sikukuu yake ya kuzaliwa akitimiza miaka 51, na amezuiliwa katika mji mkuu wa kisiasa wa Gitega.

Bunyoni, alikuwa Waziri Mkuu kuanzia katikati ya mwaka 2020 lakini aliachishwa kazi kutokana na mzozo wa ngazi ya juu wa kisiasa Septemba 2022, siku chache baada ya Rais Evariste Ndayishimiye kuonya kuhusu njama ya mapinduzi dhidi yake.

Neema yabisha hodi kwa Mabaharia wa Tanzania Kimataifa
Wanafunzi watano watekwa Nyara Chuoni