Tanzania na Burundi zimekubaliana kuendeleza ushirikiano katika kulinda rasilimali zilizopo katika Ziwa Tanganyika hatua inayolenga kuleta manufaa ya kijamii na kiuchumi baina ya mataifa hayo mawili.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo mara baada ya kumalizika kwa kikao baina yake na Waziri wa Mazingira, Kilimo na Mifugo wa Serikali ya Jamhuri ya Burundi Mhe. Prof Sanctus Niragira kilichofanyika jijini Dodoma.

Dkt. Jafo amemhakikishia Prof.Niragira kuwa Serikali ya Tanzania kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais itahakikisha inasimamia kikamilifu Mkataba wa Nchi Wanachama wa Mkatataba wa Usimamizi Endelevu wa Ziwa Tanganyika ili kuhakikisha rasilimali zilizomo zinaleta tija namanufaa kwa wananchi wa nchi
hizo mbili.

“Namshukuru Waziri mwenzangu wa Burundi kwa kuja nchini kwetu na kuona namna bora matumizi na usimamizi wa Ziwa Tanganyika ambalo linaunganisha mataifa yetu na wannachi wetu, kikao kimewakutanisha wataalamu kutoka zetu na kwa pamoja tumejadiliana na kubadilishana uzoefu wa namna ya kuhifafdhi mazingira ya ziwa letu,” amesema Dkt. Jafo.

Dodoma Jiji kuamua hatma ya Kocha Medo
Nahodha, Kocha Polisi Tanzania wakubali yaishe