Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Diane Atwine amesema Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amekutwa na maambukizi ya Uviko – 19, huku ikidaiwa kuwa yupo katika afya njema na ataendelea na majukumu yake huku akipata matibabu, amesema jana.

Katibu Mkuu huyo amesema, “Rais amepimwa na kukutwa na COVID-19. alipata dalili kama za mafua na hata hivyo yuko katika hali nzuri na anaendelea kutekeleza majukumu yake kama kawaida huku akizingatia SOPs.”

Rais Yoweri Museveni na Familia yake.

Mara baada ya kutoa kutoa hotuba ya taifa katika viwanja vya Bunge, Museveni (78), alitoa dokezo la kwanza kuwamba alikuwa ameambukizwa ugonjwa huo, akisema asubuhi alihisi baridi kidogo, na kumfanya aombe vipimo.

Hayo yalitokea baada ya vipimo viwili kati ya vitatu alivyofanya kuwa hasi, na akaongeza kuwa, “kwa hiyo mimi ni muathirika wa corona na nimesimama hapa. Ndio maana umeniona nikija kwa magari tofauti na Mama.”

Waarabu kumtajirisha Karim Benzema
Dkt. Yonaz apongeza maendeleo ujenzi Uwanja wa Mashujaa