Uongozi wa Klabu ya Dodoma Jiji wanasikilizia mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Tanzania Bara unaopigwa leo Ijumaa (Juni 09) dhidi ya Ruvu Shooting kabla ya kufanya maamuzi juu ya Kocha Mkuu wa timu hiyo kutoka Marekani, Melis Medo kama aendelee kuwepo msimu ujao au wamtupie virago.

Dodoma itakuwa ugenini kwenye Uwanja wa Jamhuri, mjini Morogoro kuvaana na Maafande hao walioshuka daraja huku kibindoni ikiwa na pointi 34 baada ya mechi 29 ikishika bnafasi ya 10.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Fred Mwakisambwa alisema wanashukuru kubaki katika ligi hiyo kwa msimu ujao kwa pointi ilizonazo sasa, ila akikiri hawakuwa na msimu nzuri kutokana na presha kubwa waliokumbana nayo.

“Uwanja wa Jamhuri haukuwa na ubora mechi saba za duru la kwanza tulicheza Singida, kwa ujumla mzunguko wa kwanza haukuwa mzuri kwetu kidogo mzunguko wa pili tumefanya vizuri hasa katika hii michezo ya mwisho,” amesema.

Mwakisambwa alifafanua kuwa, baada ya mechi ya mwisho dhidi ya Ruvu watapokea ripoti ya kocha na watakaa kuijadili na kuweka mipango ya msimu ujao kama wataendelea naye au la.

Simon Msuva: Namtakia kila la heri Fiston Mayele
Tanzania, Burundi zakubaliana ulinzi rasilimali Ziwa Tanganyika