Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva anayecheza soka la kulipwa Saudi Arabia akiwa na Al-Qadsiah, ametoa baraka zake kwa mfungaji bora wa Kombe la Shirikisho Afrika, Fiston Mayele kumaliza ukame wa miaka sita kwa Young Africans kushindwa kutoa mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara.

Msuva mwenye umri wa miaka 29, ndiye mchezaji wa mwisho kwa Young Africans kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara, alifanya hivyo msimu miwili mfululizo 2014/15 na 2015/16 kabla kwenda Morocco kucheza soka la kulipwa.

Nyota huyo wa zamani wa Wydad Casablanca ya Morocco, anaamini Mayele ni kati ya washambuliaji bora Afrika hivyo yupo na ubora wa kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara licha ya kuwa na upinzani kutoka na Said Ntibazonkiza.

“Nadhani hata msimu uliopita alikuwa na nafasi hiyo ila bahati haikuwa upande wake, ni mchezaji mzuri na mwenye uwezo wa kufunga, uwepo wake na wachezaji wengine wa kigeni ambao wanafanya vizuri wanaamsha ari kwa wazawa,” amesema Msuva na kuongeza:

“Yupo na nafasi ya kuwa mfungaji bora japo mchezo mmoja unaweza kubadili mambo, nikiri pia navutiwa sana na uchezaje wake,”

Msimu wa mwisho akiwa Young Africans, Msuva alimaliza kinara akifunga mabao 14 sawa na Abdulrahman Mussa.

Rais Dkt. Samia afungua Mkutano Baraza la Taifa la Biashara
Dodoma Jiji kuamua hatma ya Kocha Medo