Hospitali ya Benjamin Mkapa – BMH, imeanza kambi ya upasuaji wa moyo kwa watu wazima.

Daktari Bingwa wa Moyo wa BMH, Dkt. Kelvin Masava, amesema kambi hiyo ya pamoja ya wiki moja kati ya wataalam wa BMH na wenzao kutoka Uholanzi, itahusisha vipimo na matibabu kwa njia ya upasuaji wa kufungua kifua.

Amesema, “mpaka sasa tuna wagonjwa 450 ambao watafanyiwa uchunguzi, watakaokutwa na matatizo watapatiwa matibabu,” amesema Daktari huyo Bingwa wa Moyo na kufikia sasa wamewafanyia uchunguzi wagonjwa 146 na wagonjwa wawili wamenufaika na huduma ya upasuaji wa kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo kwa mishipa iliyoziba bila kuusimamisha moyo “Off-pump Coronary Artery Bypass surgery.”

Dkt. Masava ametoa wito kwa watu wazima wenye matatizo ya moyo katika Kanda ya Kati na mikoa ya jirani waitumie kambi hii ya matibabu katika BMH kwa ajili ya kupata suluhisho.

Aidha, ameongeza kuwa lengo la kambi hii ya pamoja na wenzao wa Uholanzi ni kutoa huduma pamoja na kubadilishana uzoefu.

Tanzania yatarajia kukuza uchumi kwa kasi Duniani - ILO
Wakutana kujadili uridhiaji Mikataba ya ILO