Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Patrobas Katambi amewataka Walimu kuwaweka wazi Watumishi wa Serikali wanao wakwamisha na wanao wanyanyasa, ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa dhidi yao.
Katambi ametoa kauli hiyo Jijini Dodoma wakati akifungua kongamano la walimu wanawake taifa huku akiongeza kuwa Serikali haiwezi kukubali kuona walimu wakinyanyasika na watu wachache.
“Sasa hawa wakwamishaji ambao tayari mmewataja popote pale nchini kwasababu kuna uwakilishi wa viongozi wa wanawake walimu mikoa lakini pia tunacho chama cha walimu ambacho ni chama kubwa kiko kila mahali, kama watu hao wanaowasumbua wali wetu wapo nitaomba tupewe majina yao awe ni Naibu Waziri kwasababu ni mtumishi wa umma na msimamizi namba moja wa shughuli za umma ni Rais na hakuna mahali amesema walimu wanyanyasike,” amesema.
Amesema Walimu ndiyo msingi mkuu wa maendeleo kwa taifa lolote ulimwenguni na hakuna maendeleo ambayo yatapatikana kama raia wake watakuwa hawana elimu yenye maarifa na ujuzi, vivo hivyo kwa walimu hao tena wakina mama ndiyo viongozi wakuu wa familia hivyo huo ni ujumbe kuwa hawa ni watu ambao wanafanya utimilifu wa kazi ya Mungu.
“Taifa letu leo tunazungumza tuna wataalam mbalimbali kweye nyadhifa tofauti tofauti bila ya kuwa kuna sehemu walipita wakapatiwa maarifa na ujuzi wa kufanya haya ambayo leo tunayashuhudia ingekuwa ni kazi bure, kwahiyo walimu niendelee kuwashukuru na kuwapongeza juu ya kile mnachokifanya ndiyo maana Mwalimu Nyerere alipenda sana kuitwa mwalimu kuliko vyeo vingine vyovyote ni kutokana na kazi kubwa amabyo mnaifanya,” aliongeza Katambi.
Aidha, amewashukuru waandaji wa kongamano hilo ambalo wameliasisi na kuwapa viongozi nafasi wa kitengo cha wanawake walimu kujitathmini kwenye hatua ambazo zinmepigwa na chama cha walimu katika kushughulikia haki na maslahi ya walimu hususani walimu wanawake.
“Ni hatua kubwa ambayo sisi kama Serikali tunaiona kwamba ina tija kubwa kwasababu bila kujua changamoto zenu na kinacho wasibu na kuwa na karibu na mfumo wa kiuongozi namna hii ni ngumu kuweza kutatua changamoto zenu na matakumbuka katika kipindi cha nyuma kulikuwa na migogoro mingi na migomo ya walimu kwamba hii inatoakana zaidi na kukosa nidhamu lakini nidhamu hii lazima tukubaliane pia inawezekana tunatamani walimu wawe na nidhamu lakini upande wa Serikali hatutimizi wajibu wetu,” ameongeza.
Katambi pia amegusia suala la maadili kwa kusema wanapaswa kukabiliana nalo kwani ni jambo la msingi ambalo linapaswa kutiliwa mkazo ili kupata viongozi imara.
Awali, Makamu wa Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Suleiman Abdallah amewaomba watanzania kuacha kuwabeza walimu kwa makosa ya mtu mmoja anayetaka kuchafua taswira ya walimu.
“Kama kuna mtu anatamani kuwabeza walimu basi anatukose sana kwasababu ndiyo kada ambayo inashughulika na maisha ya mwananchi mmoja mmoja kupitia familia au watoto wake,” amesema.
Pia amemuhakikishia Naibu Waiziri Katambi kuwa kile chama ambacho kilikuwa kinafikirika kuwa kuna mambo yake hayaendi na kipo katika mamlaka yake basi CWT si kile na yaliyopita tayari yamepita na kwasasa ni chama imara na wale wazushi wazushi wameendelea kuwapunguza ambao wamekuwa wakianzisha uchonganishi.
Akisoma risala ya Walimu Wanawake Taifa, Mwakilishi wa Walimu Elizabeth Walema amesema kongamano hilo limeandaliwa kwaajili ya kuwajengea uwezo na viongozi na kukuza stadi za mbinu katika masuala ya uongozi, kuwawezesha kuwa na uelewa wa pamoja katika usiamamizi na utekelezaji wa sera za jinsia na walimu wanawake, kuimarisha masuala ya ushawishi, mbinu za mawasiliano ili mkuleta ufanisi na madiriko chanya katika chama chao pamoja na kuimarisha ushirikiano na uwajibikaji.