Mwanamuziki, John Legend amezua gumzo baada ya kupiga debe la mwisho kwa mgombea anayemuunga mkono wakati Wamarekani wakiendelea na zoezi la kupiga kura kumchagua Rais wa nchi hiyo.

Mwimbaji huyo wa ‘All of Me’ alipost kipande cha video kwenye twitter akimponda mgombea wa Republican, Donald Trump kuwa hafai kuwa Rais wa nchi hiyo, huku akimpigia chapuo Hillary Clinton wa Democratic.

“Donald Trump is unfit for the office of president. Fortunately, there’s an exceptionally qualified candidate @HillaryClinton,” alitweet.


Ndani ya sekunde chache, ukurasa wake ulitawaliwa na maoni makali ya mashabiki wake, wengi wakimkosoa kwa alichokiandika.

Kwa wastani, watu wanaomuunga mkono Trump ndio walioongoza kwa idadi ya waliomkosoa vikali Mwimbaji huyo. .

Haya ni baadhi ya maoni hayo:

12345

Tanzia: Mungai afariki Dunia
Video: Wabunge wakubali msimamo wa Serikali