Waziri wa Elimu wa zamani, Joseph Mungai amefariki dunia leo jioni jijini Dar es Salaam.

Mtoto wa marehemu ameeleza kuwa baba yake amefariki majira ya jioni wakati akipelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kutapika ghafla kwa muda mrefu.

 

Mtoto huyo wa Marehemu ameviambia vyombo vya habari kuwa Marehemu Mungai alianza kutapika ghafla baada ya kula chakula ambacho hakikuwa salama.

Taarifa za kifo cha Mungai zimekuja wakati Tanzania ikiendelea kuomboleza kifo cha aliyewahi kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samuel Sitta.

Dar24 inaungana na Watanzania wote katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na wapendwa wetu, waliowahi kushika nyadhifa za juu za Uwaziri.

Majaliwa aiomba uingereza kuwekeza zaidi nchini
John Legend azua kizaazaa kwa kumpigia 'debe la mwisho' mmoja kati ya Trump na Clinton