Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi, amemuandama Mtendaji wa Mtaa wa Mizimuni katika manispaa ya kinondoni, Shabani Kambi kwa kosa la kutosimamia mfumo wa uzoaji taka katika mtaaa huo.
Pia amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Aron kagulumjuli kutoa magari yote yaliyopaki katika mitaa ya wilaya yake kinyume na sheria.
Akitoa maagizo hayo Dar es salaam jana baada ya Mtendaji wa kata hiyo kushindwa kutoa taarifa sahihi kuhusu makusanyo ya ushuru na utoaji taka, Hapi alisema Mtendaji wa mtaa anapaswa kujua mapato ya mtaa wake na kutoa taarifa iliyokamilika na si nusu nusu.
Alisema kila mwananchi anatakiwa kufuata utaratibu uliowekwa na mtaa na si kuacha serikali kufawafanyia kazi.
Alli hapi amesema, ” Mtendaji umeonesha upungufu mkubwa wa kutojua makusanyo ya mapato ya ukusanyaji taka yanayotolewa na wananchi ni lazima Mtendaji na Ofisa Afya, kusimamia taratibu za sheria zilizopo na si kuwaacha wananchi kutolipa ushuru wa taka”.
Pia kupitia taarifa hizo finyu Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni alitoa tamko kwa wakazi wa manispaa hiyo kwamba wanachi wote wanaozalisha taka ni wajibu wao kulipia ushuru, endapo ukaidi utajitokeza katika hilo, mwananchi husika akamatwe na na kulipishwa faini na kupelekwa katika mahakama ya jiji.
Hapi alimaliza kwa kusema ”Tunataka kujenga jamii yenye nidhamu .”