Aliyekua kocha mkuu wa timu ya taifa ya Afrika kusini Ephraim ‘Shakes’ Mashaba amepoteza rufaa yake iliyokua inawazuia viongozi wa chama cha soka nchini humo (SAFA) kuendelea na mchakato wa kumsaka mkuu wa benchi la ufundi.

Mashaba alikata rufaa ya kupinga maamuzi yaliyochukuliwa dhidi yake mwishoni mwa mwaka jana kwa kuhisi alionewa, lakini mahakama ya kazi Afrika kusini imeonea rufaa ya kocha huyo haina uzito.

Maamuzi hayo yanaipa meno SAFA kuendeleza na mchakato wa kumsaka kocha mpya ambaye atakabidhiwa majukumu ya kuipelekea Afrika kusini kwenye fainali za kombe la dunia 2018 na zile za Afrika za 2019.

Tayari SAFA wameshatangaza kuwa katika hatua za mwisho kukamilisha mchakato wa kumtangaza kocha mpya, ambapo taarifa ya mwisho ilieleza huenda mwishoni mwa mwezi huu wakahitimisha jambo hilo.

Mashaba alipoteza kibarua chake mwishoni mwa mwaka jana baada ya kupishana kauli na waajiri wake (SAFA), na sababu kubwa ilikua ni kushindwa kuipeleka Bafana Bafana kwenye fainali za Afrika za 2017 ambazo ziliunguruma nchini Gabon na Cameroon kutwaa ubingwa.

Hapi atoa onyo, usimamizi mbovu uzoaji taka
Man Utd Yaacha Athari Ewood Park