Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein amemtaka Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kuikosoa Serikali yake pasipo kuvunja sheria za nchi.
Ameyasema hayo Ikulu ya Zanzibar wakati akiadhimisha mwaka mmoja tangu alipoingia madarakani kupitia uchaguzi wa marudio wa Machi 20 mwaka jana, Dkt Shein amesema kuwa, Maalim Seif Hamad ana uhuru wa kusema akitakacho wakati wowote, lakini asitumie lugha za matusi.
Aidha, Dk Shein amesema kuna maneno mengi yamekuwa yakisemwa mitaani juu ya kuwapo kwa Serikali nyingine badala ya anayoiongoza, kauli ambapo amesemakuwa kauli hizo hazina mashiko.
Hata hivyo, Shein amezitaja njia za kupata Serikali kuwa ni mbili tu duniani kote, ambapo amesema kuwa moja ni ya kupigiwa kura na nyingine ni ya kufanya mapinduzi kwa upande unaohisi umeonewa.