Rais wa Marekani, Donald Trump amemtaka Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro kurejesha hali ya amani katika nchi hiyo iliyoingia machafuko ya kisiasa hivi karibuni, akitaka kurejeshwa kwa demokrasia na uhuru wa kisiasa nchini Venezuela.

Akizungumza na viongozi kutoka Amerika ya kusini Jijini New York, Rais Trump amesema kuwa atachukua hatua kali zaidi dhidi ya kile alichokiita utawala wa kidikteta wa Rais Nocolas Maduro.

Aidha, amesema kuwa watu wa Venezuela wamekuwa wakikosa mahitaji muhimu kama chakula na kila kukicha nchi hiyo inazidi kuharibika licha ya awali kuwa nchi tajiri ya yenye kuvutia watalii lakini kwa sasa machafuko hayo yameharibu kila kitu.

Hata hivyo, Mwezi uliopita serikali ya Marekani iliiwekea vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Venezuela, huku ikitishia kutaifisha mali za Rais Nicolas Maduro zilizopo nchini Marekani kwa kile ilichokiita kukomesha udikteta wa Rais Maduro.

 

Israel na Marekani zaunda kambi ya pamoja ya jeshi la anga
Bob Junior awashambulia wanaoingilia 'beef' lake na Diamond, asema hawajui undani wa tatizo