Orodha ya awali ya wanaowania tuzo ya mpira wa dhahabu (Ballon d’Or) imetangazwa muda mchache uliopita, huku kiungo wa mabingwa wa soka nchini England Chelsea N’Golo Kante, akiwa miongoni mwa waliotajwa.

France Football, ambao wanaratibu tuzo hizo baada ya kuvunja ushirikiano na shirikisho la soka duniani FIFA uliokuwepo siku za nyuma, wametangaza orodha hiyo ya awali na baadae wataichuja na kusaliwa na wachezaji watatu.

Kante ni mchezaji pekee anayecheza ligi ya nchini England alieanza katika orodha hiyo, na sababu kubwa ya kuingia kwenye mchakato huo, ni juhudu kubwa aliyoionyesha msimu uliopita ya kuisaidia Chelsea kutwaa ubingwa wa EPL.

Mshambuliaji mpya wa PSG na nahodha wa timu ya taifa ya Brazil Neymar, naye ametajwa katika orodha hiyo sambamba na beki wa pembeni wa mabingwa wa soka nchini Hispania Real Madrid  Marcelo, kiungo Luka Modric na mshambuliaji kutoka nchini Argentina na klabu ya Juventus Paulo Dybala.

Orodha ya awali ya wachezaji wanaowania tuzo ya Ballon d’Or iliyotangazwa.

Neymar (PSG/Brazil), Luka Modric (Real Madrid/Croatia), Paulo Dybala (Juventus/Argentina), Marcelo (Real Madrid/Brazil), N’Golo Kante (Chelsea/France).

France Football wana orodha ya wachezaji 30, na tayari wametangaza majina ya wachezaji watano, hivyo orodha nyingine ya wachezaji 25 inatarajiwa kutangazwa baadae hii leo.

Kwa saa za England orodha nyingine itatangazwa saa 11:00, 13:00, 16:50, 17:35 na 18:15.

Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo, ndio mshindi wa tuzo ya mpira wa dhahabu kwa mwaka 2016, na anatarajiwa kuwa miongoni mwa wachezjai watakaotajwa baadae sambamba na mpinzani wake wa karibu Lionel Messi.

 

@@@@@@@@@@@@@@@

N'Golo Kante aondoka kambini Ufaransa
Huyu ndiye mchezaji atakayevunja rekodi kombe la dunia 2018