Mshambuliaji wa klabu ya Liverpool Mohamed Salah amekata kiu ya Misri iliyodumu kwa miaka 27 baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Kongo na kuifanya timu yake kufuzu kucheza kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi.

Misri imefuzu kwenda fainali za kombe la dunia kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1990, mkwaju wa penati ya mguu wa kushoto wa Salah katika dakika ya nne ya muda wa nyongeza ilileta ushindi uliokuwa ukisubiriwa na mashabiki wa nchi nzima.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Chelsea na timu ya taifa ya Ivory Coast, mkongwe Didier Drogba amemtumia ujumbe wa pongezi Mohamed Salah kwa kuliwezesha taifa lake kufuzu kombe la dunia.

Misri imekuwa nchi ya pili kufuzu kwa ajili ya fainali za kombe la dunia 2018 nchini Russia baada ya Nigeria kujihakikishia nafasi siku ya Jumamosi.

Ushindi huo umepelekea maelfu ya mashabiki kujazana kwenye mita ya Misri wakisherekea huku wakipeperusha bendera za taifa lao.

Katikati ya jiji la Cairo helicopter ya kijeshi ilikuwa ikidondosha mamia ya bendera za nchi hiyo kwa mashabiki waliokuwa barabarani wakishangilia kwenye sehemu maarufu inayofahamika kwa jina la Tahrir square.

Huyu ndiye mchezaji atakayevunja rekodi kombe la dunia 2018
Video: JPM awaapisha mawaziri wapya