Mhasibu mmoja nchini Italia anayeitwa Valentino Talluto amefungwa jela miaka 24 kwa kuwaambukiza virusi vya Ukimwi kwa makusudi wanawake 30.

Valentino Talluto anadaiwa kushiriki mapenzi bila kinga na wanawake wanaofikia 53 baada kugundulika kuwa na virusi vya ukimwi mwaka 2006, mwanamke mdogo katika hao akiwa na miaka 14.

Mhasibu huyo ambaye alikuwa anatumia mitandao ya kijamii na tovuti za kuchumbiana kuwawinda wanawake na mara zote wanawake walipomgundua alikanusha madai kwamba alikuwa na virusi hivyo ambavyo husababisha Ukimwi.

Pamoja na mawakili wa Talluto kumtetea mteja wao wakisema vitendo vyake havikuwa vya busara, lakini havikuwa makusudi Ijumaa jaji alimhukumu Talluto mwenye umri wa miaka 33 kifungo cha miaka 24 jela.

Talluto alijitetea kwamba wanawake wote aliokuwa nao alikuwa na mahusiano nao ya kimapenzi na kwamba lengo lake halikuwa kuwaambukiza virusi.

“Wanasema kwamba nilitaka kuwaambukiza Ukimwi watu wengi zaidi. Kama lingekuwa ndio lengo langu ningeenda basi kwenye baa na kushiriki ngono kiholela nisingewaingiza katika maisha yangu” alisema Tallulo

Mama yake Talluto alikuwa anatumia madawa ya kulevya na aliuambukizwa pia virusi vya Ukimwi nakufariki Talluto akiwa na miaka minne.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari Italia, mhukumiwa alilia hukumu ilipokuwa inasomwa hata hivyo, adhabu hiyo haikufikia hukumu ya kufungwa jela maisha ambayo viongozi wa mashtaka walikuwa wameomba mahakama ahukumiwe.

Video: Tambo za mashabiki kuelekea mchezo wa watani wa jadi Yanga na Simba leo
Video: DC Hapi awataka wanaoishi mabondeni wahame