Leo siku ya Jumamosi October 28, 2017 hakika hatumwi mtoto dukani kwani ule mpambano wa watani wajadi katika soka la Tanzania, Yanga na Simba wanatarajia kumenyana katika uwanja wa Uhuru kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara VPL.

Mashabiki wa timu zote mbili wamekuwa na maoni na tambo tofauti huku wakijivunia vikosi vya timu zao kuwa imara kuweza kuibuka na ushindi katika mchezo huo.

Hawa ni baadhi ya mashabiki kutoka matawi ya Yanga na Simba Kawe na Tegeta jijini Dar es salaam wakitoa maoni yao katika viedeo hii hapa chini;

Anthony Martial aivunja Tottenham
Aliyesambaza Ukimwi kwa makusudi afungwa jela miaka 24