Anthony Martial ameifungia Manchester United bao pekee lililoifanya klabu hiyo kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tottenham katika mchezo wa kukata na shoka ulipoigwa kwenye dimba la Old trafford.

Martial aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Marcus Rashford amefunga bao hilo dakika ya 81 ya mchezo huo baada ya kupata pasi nzuri ya kichwa kutoka kwa Romelu Lukaku na Matrial kupachika mpira kimiani kwa ustadi mkubwa.

Tottenham wakicheza bila mshambuliaji wao Harry Kane walipata nafasi ya kufunga bao lakini Dele Alli alipiga shuti ambalo lilienda nje ya lango.

Kwa ushindi huo Manchester United wamefikisha jumla ya pointi 23 wakiwa nafasi ya pili nyuma ya vinara Manchester City wenye pointi 25 wakitarajia pia kushuk dimbani badae kumenyana na West Bromwich Albion.

Anthony Joshua na Carlos Takam kupanda ulingoni usiku wa leo
Video: Tambo za mashabiki kuelekea mchezo wa watani wa jadi Yanga na Simba leo