Bingwa wa mkanda wa WBA na IBF katika uzito wa juu duniani Anthony Joshua anatarajia kupanda ulingoni leo kuzipiga na bondia Carlos Takam amabye ni raia wa Cameroon leo mjini Cardiff.

Pambano hilo litakalopigwa katika uwanja wa Principality litakuwa pambano ambalo litatazamwa na idadi kubwa ya watu, mashabiki wapatao 70,000 wakitarajiwa kulishuhudia pambano hilo.

Joshua alikuwa na uzani wa 18st 2lbs wakati alipopimwa siku ya Ijumaa ,ukiwa ni uzani mzito zaidi katika pigano huku Takam naye akiwa na uzani wa 16st 11bs.

Raia huyo wa Uingereza anasema kuwa ana hamu zaidi ya kushinda pambano hilo zaidi ya lile alilopigana na Wladmir Klitschko katika uwanja wa Wembley mnamo mwezi Aprili.

Antony Joshua alitakiwa kupambana na Kubrat Pulev lakini bondia huyo raia wa Bulgaria alipata majereha ya bega wakati akijiandaa na mchezo huo.

 

Video: Takwimu za mapato zinazotangazwa na Serikali si sahihi- Zitto Kabwe
Anthony Martial aivunja Tottenham