Kiongozi wa chama cha upinzani kaskazini mwa nchi ya Cameroon, Aboubakar Siddiki amehukumiwa kwenda jela miaka 25 kwa makosa ya kuchochea uasi.

Shirika la haki za binadamu la Amnesty International limeikosoa mahakama ya kijeshi nchini Cameroon kwa kumhukumu kiongozi huyo miaka 25 jela kwa makosa ya uasi likidai hakuna ushahidi uliotolewa mahakamani kuchangia hukumu kama hiyo.

Aboubakar Siddiki alikamatwa mwaka 2014 baada ya kudaiwa kupanga njama za kuipindua serikali iliyo madarakani ya Rais Paul Biya.

Rais wa Cameroon Paul Biya amekuwa madarakani tangu mwaka 1982 na wapinzani wake wengi wanamtaja kuwa dikteta.

Rais wa Cameroon Paul Biya

Aboubakar Siddiki

Watu kadhaa wameuawa na mamia kukamatwa wakati wa maandamano katika eneo hilo lenye watu wanaozungumza lugha ya Kiingereza na ambao wanalalamika kutengwa.

Magazeti ya Tanzania leo Novemba 1, 2017
Moses Basena aomba kupandishwa cheo Uganda