Nahodha wa Real Madrid Sergio Ramos ameachwa kwenye kikosi kilichosafiri kwenda nchini Cyprus kucheza na Apoel Nicosia leo kwenye mchezo wa hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Ulaya.
Ramos aliumia pua kwenye mchezo wa La Liga jumamosi iliyopita wakati timu yake ya Real Madrid ilipotoka sare ya bila kufunagana na Atletico Madrid kwenye uwanja wa Wanda Metropolitano.
Aidha, Mlinzi huyo wa kati mwenye miaka 31, bado haijajulikana atarejea lini uwanjani, huku akiongeza idadi ya majeruhi kwenye timu hiyo akiwemo winga Gareth Bale pamoja na golikipa Keylor Navas.
Mabingwa hao watetezi wa UEFA wameshinda mechi moja tu katika michezo yao minne iliyopita kwenye mashindano yote.
Hata hivyo, Katika kundi H Real Madrid ina nafasi nzuri ya kufuzu hatua ya 16 bora pamoja na timu ya Tottenham Hotspurs ambayo itakuwa ugenini leo nchini Ujerumani kukipiga na wenyeji Borussia Dortmund.