Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Lazaro Mambosasa amekanusha taarifa zinazosema kesi ya Dkt.Louis Shika imetupiliwa mbali, na kusema kwamba kesi yake bado ipo pale pale isipokuwa hawajaipa kipaumbele.

Akizungumza na waandishi Kamanda Mambosasa amesema jalada la kesi ya Dkt. Shika bado lipo isipokuwa kesi yake haina mashiko kwani hajaleta madhara yoyote kwenye nyumba zilizokuwa zikipigwa mnada.

Kamanda Mambosasa amesema iwapo wataamua kumpandisha mahakamani Dkt. Shika kujibu mashitaka yake umma utajulishwa ili wajue kile kinachoendelea.

“Siyo kweli kama tumeamua kuachana naye kabisa, jalada lake lipo na likikamilika tutaamua nini kinafuata, Shika hakuleta madhara yoyote hivyo kesi yake haina public interest, nyumba ziko salama na hajadhuru mtu, tukiamua kumpandisha mahakamani tutaujulisha umma ili wajue”, amesema Kamanda Mambosasa.

Dkt. Louis Shika amefunguliwa jalada la kesi kwa kosa la kuharibu mnada wa nyumba za Lugumi ambao upo kwa amri ya serikali, kwa kusema ananunua nyumba hizo kwa milioni 900 ilihali mfukoni hana pesa kabisa.

 

Majaliwa: Rais Magufuli kuhamia Dodoma mwakani
Raila Odinga aonywa vikali kujiapisha