Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma limewataka wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi pindi wanapo wakamata waarifu na kuwataka kufuata sheria kwa kuwapeleka sehemu husika itakayo wawajibisha kwa mujubu wa sheria.
Akizungumza na Dar 24 Media, Kamanda wa Polisi ACP Simon Marwa Maigwa amesema kuwa kitendo hicho cha kujichukulia hatua mikononi ni uvunjaji wa sheria lakini pia inaweza kusababisha kukosa mtandao wa taarifa za waarifu wengine kupitia mtuhumiwa aliyekamatwa endao watamdhuru kwa kumpiga mpaka kufa.
Hayo yamejiri baada ya wananchi katika eneo la Mauki kata ya Msamala Manispaa ya Songea Mkoa wa Ruvuma baada ya kumjeruwi mwanaume anaekadiriwa na umri wa miaka 45-50 kwa tuhuma za uwizi.
Aidha Kamanda Marwa amesema kuwa Jeshi la Polisi Ruvuma wamejipanga kutoa elimu kwa wananchi kutokujichukulia sheria mikononi endapo watamkamata muharifu, lakini pia amewahasa kila mwananchi kuwa balozi kwa mwenzake katika kuelimishana.
Sambamba na hayo kuelekea sikukuu ya Eid El Fitr Kamanda Marwa amesema Jeshi la Polisi limejipanga kikamilifu kusimamia usalama kwa wananchi, na kuwahasa pia wananchi kuwa makini hasa kwa upande wa kuwalinda watoto na watu kuwa makini katika vivuko barabarani.