Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Merisone Mwakyoma amethibitisha kutokea kwa tukio la nyumba kuchomwa moto na mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Heriko huku Felister Michael akinusurika kifo katika tukio hilo lililotokea katika kijiki cha Wama, Kata ya Gisalamba Wilayani Hanang huku sababu ikitajwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Kamanda Mwakyoma amesema kuwa uchunguzi wa awali umebaini kwamba mtuhumiwa Heriko alimnunulia pombe mpenzi wake Felista kwa makubaliano ya kuondoka naye lakini baadaye mwanamke huyo aliondoka na mwanamme mwingine ambaye naye alielezwa kumnunulia pombe pia, jambo ambalo lilimtia hasira Heriko na kuamua kwenda kuichoma nyumba ya mpenzi wake huyo.

Katika tukio jingine, mtu mmoja anayefahamika kwa majina ya Isaka Yustin mwenye umri wa miaka 27 mkazi wa kijiji cha Emango kilichopo Kata ya Galapo wilaya ya Babati Mkoani Manyara ameuawa na aliyekuwa mkewe kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali shingoni. 

Jeshi la Polisi mkoani Manyara bado linaendelea na uchunguzi kufuatia matukio hayo ya kinyama.

Live: Rais Samia akiwasili uwanja wa Ndege akitokea Nchini Marekani
Bilioni 30 kujenga kituo cha biashara na lojistiki