Mshambuliaji kutoka nchini Togo, Emmanuel Adebayor pamoja na meneja muingereza Tim Sherwood wanatarajia kufanya kazi kwa pamoja kwa mara nyingine tena baada ya wawili hao kufikia makubaliano rasmi.

Adebayor mwenye umri wa miaka 31 atatimiza ndoto za kufanya kazi na meneja huyo kufuatia uongozi wa klabu ya Aston Villa kufunguliwa milango ya kumsajilia kitokea Tottenham Hotspurs.

Jana jioni taarifa zilidai kwamba, Adebayor alitarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya yake kabla ya kukamilisha utaratibu wa kujiunga na klabu ya Aston Villa.

Sherwood, alimuweka Adebayor katika orodha ya wachezaji aliokua na mipango ya kufanya nao kazi tangu alipokubalia kumuachia Christian Benteke aliyetimkia kwa majogoo wa jiji Liverpool.

Mshahara wa Adebayor unatajwa kuwa paund 100,000 kwa juma endapo atakamilisha mikakati ya kuelekea Villa Park, huku Spurs wakiweka hadharani kiasi cha paund million 5 ambacho ni ada yake ya usajili.

Mipango ya kusajiliwa kwa Adebayor, iliibuka saa chache baada ya uongozi wa Aston Villa kukamilisha usajili wa mshambuliaji kutoka nchini Ghana Jordan Ayew akitokea Lorient nchini Ufaransa kwa ada ya uhamisho wa paund million 8.5.

Benzema Awapandisha Mzuka Mashabiki Wa Arsenal
Mzee Ojwang kuzikwa leo, Mastaa wa Kenya wajiandaa na Show