Mshambuliaji kutoka nchini Ufaransa, , Karim Mustapha Benzema amewapandisha mzuka mashabiki wa Arsenal, baada ya kuandika ujumbe mzito katika mtandao wa kijamii wa Twitter na kuweka picha ikimuonyesha yupo katika ndege ya kukodi.

Benzema, mwenye umri wa miaka 27, hakusafiri na kikosi cha Real Madrid ambacho kimeweka kambi ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi huko nchini China aliandika, kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter “Tuache yaliyopita kuwa yaliyopita. #Muelekeowamaishayabaadae.

Mshambuliaji huyo amekuwa akihusishwa na mipango ya kutaka kujiunga na klabu ya Arsenal kwa majuma kadhaa sasa, huku ikiripotiwa huenda akaelekea jijini London kwa zaidi ya paund milioni 30.

Madai mengine yamekuwa yakiendelea kuchagiza usajili wa Benzema huko kaskazini mwa jijini London, ni kuachwa kwa jezi namba tisa ambayo haitumiwi na mchezaji yoyote kwa sasa, huku ikielezwa kusudio la kufanywa hivyo ni kwa ajili ya kutimiza azma ya mshambuliaji huyo ambaye amekua akipendezwa na namba hiyo kuweka katika vazi lake la uwanjani.

Karim Djaziri, wakala wa Benzema juma lililopita aliwaeleza mashabiki wa soka duniani kupitia kituo cha televisheni cha Sky Sports cha nchini Uingereza kwamba, mshambuliaji huyo ambaye aliwahi kuitumikia klabu ya Olympic Lyon, ataendelea kuwa mchezaji wa Real Madrid kwa asilimi 1000, kama mkataba wake unavyoonyesha.

Hata hivyo, meneja wa Arsenal, Arsene Wenger alipoulizwa juu ya kauli hiyo alijibu inawezekana kwa Benzema kuendelea kubaki Real Madrid hadi mwishoni mwa mkataba wake, lakini yeye kama meneja mzoefu katika soka la barani Ulaya anaichukuliwa kauli hiyo ya wakala wake kama utani.

 

Maelezo Ya Kina Kuhusu Job Ndugai Kumshambulia Kada Wa CCM Kwa Fimbo
Adebayor Anukia Aston Villa Ya Tim Sherwood