Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ limemteua Afisa Habari na Mawasilino wa Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’ Clifford Mario Ndimbo, kuwa Ofisa Habari wa mchezo wa Hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) kati ya Simba SC (Tanzania) dhidi ya Vipers (Uganda).

Simba SC itakuwa mwenyeji wa mchezo huo wa mzunguuko wanne wa Kundi C, utakaopigwa Jumanne (Machi 07), katika Uwanja wa Benjamin Mkapa saa kumi jioni.

Taarifa iliyochapishwa kwenye Vyanzo vya Habari vya TFF imeleeleza: “Ofisa Habari na Mawasiliano TFF, @clifordmariondimbo ameteuliwa na CAF kuwa Ofisa Habari wa mchezo wa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) Simba SC (Tanzania) vs Vipers (Uganda) utakaochezwa Machi 7, 2023 Uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam.”

Simba SC italazimika kushinda mchezo huo ili kuendelea kufufua matumaini ya kutinga Hatua Robo Fainaili, baada ya kufanya hivyo nchini Uganda mwishoni mwa juma lililopita kwa kuifunga Vipers SC 0-1.

Msimamo wa Kundi C hadi sasa, Raja Casablanca ya Morocco inaongoza ikiwa na alama 09, ikifuatiwa na Horoya AC ya Guinea yenye alama 04, Simba SC inashika nafasi ya tatu kwa kuwa na alama 03 na Vipers SC inaburuza mkia ikiwa na alama 01.

Urusi yaingilia kati sakata la ushoga Kenya, yaonya umagharibi
Rais Mteule atoa wito kwa wapinzani