Watu wengi hawajui faida ya kula ndizi mbivu, lakini ulaji wa ndizi mbivu ni zaidi ya ulaji wa Tunda kwa ajili ya afya ya mwili na pia tiba kwa ajili ya baadhi ya magonjwa yanayotupata sisi wanadamu.

Ndizi ina aina tatu za kipekee za sukari zinazojulikana kitaalamu kama Sucrose, Fructose na Glucose na vile vile ina kiasi kingi cha ufumwele (fibre), ambacho husaidia sana katika usagaji wa chakula tumboni.

Ndizi ina uwezo mkubwa wa kuongeza na kuimarisha nishati ya mwili, unaweza kupata nishati ya kufanya kazi au mazoezi ya muda wa dakika 90 kwa kula ndizi mbili tu, ni tunda muhimu sana kwa wanamichezo na ni tunda lenye uwezo pia wa kuponya na kuzuia matatizo mengi ya kiafya, na zifuatazo ni faida za kula ndizi mbivu.

Mfadhaiko wa akili – Depression.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Chama Cha Taifa cha Afya ya Akili – MIND cha nchini Uingereza, watu wanaosumbuliwa na tatizo la mfadhaiko wa akili, wengi wao waliondokana na tatizo hilo na kujisikia vizuri baada ya kula ndizi mbivu.

Hali hii inatokana na ukweli kwamba ndizi ina kirutubisho kinachojulikana kama tryptophan, ambacho ni aina fulani ya protini inayotumika mwilini kumfanya mtu kuwa mtulivu na mwenye furaha.

Matatizo wakati wa Hedhi – PMS.

Kama wewe ni miongoni mwa wale akina mama wanaopatwa na matatizo mbalimbali ya kiafya wakati wa hedhi, unashauriwa kula ndizi mbivu na unaweza kupona. Vitamin B6 iliyomo kwenye ndizi, hurekebisha kiwango cha sukari ambacho huweza kuathiri hali ya mtu.

Upungufu wa Damu – Anaemia.

Ndizi ikiwa ni chanzo kizuri cha madini aina ya chuma (iron), inaweza kuwa ni dawa ya kuzuia na kuponya upunguvu wa damu kwa sababu madini ya chuma huamsha uzalishaji wa chembechembe za damu mwilini.

Shinikizo la Damu – Blood Pressure.

Tunda hili ni la aina ya kipekee, lina kiwango kikubwa cha madini ya potasiamu (potassium) na wakati huo huo lina kiasi kidogo sana cha chumvi (sodium), hivyo kulifanya kuwa tunda bora katika kupambana na tatizo la kupanda na kushuka kwa shinikizo la damu.

Ukweli huo, hivi karibuni umeifanya Mamlaka ya Dawa na Chakula ya nchini Marekani, iwaruhusu wazalishaji na wauzaji wakubwa wa ndizi nchini humo, kutangaza rasmi uwezo wa ndizi katika kupambana na hatari ya shinikizo la damu na kupatwa na kiharusi (stroke) kwa binadamu.

Nguvu ya Akili – Mental Strength.

Hivi karibuni, wanafunzi wapatao 200 wa Shule ya Twickenham nchini Uingereza, walisaidiwa kufaulu mitihani yao kwa kula ndizi mbivu wakati wa mlo wa asubuhi (breakfast), wakati wa mapumziko na wakati wa chakula cha mchana, ndizi ziliongeza uwezo wa akili zao.

Utafiti unaonesha kuwa, potasiamu iliyojazana kwenye ndizi, ina uwezo wa kumsaidia mwanafunzi kuamsha uwezo wake wa kujisomea.

Mning’inio – Hangovers.

Moja ya dawa ya haraka ya kuondoa uchovu unaotokana na ulevi wa jana yake (hangover), ni kunywa ‘Milkshake’ iliyotengenezwa kwa ndizi na kutiwa asali.

Ndizi hutuliza tumbo, ikisaidiwa na asali, hurejesha kiwango cha sukari kilichopungua kwenye damu, wakati maziwa hutuliza na kurejesha maji kwenye mfumo wake.

Vidonda vya Tumbo – Ulcers.

Sio tu kwamba ndizi hupambana na seli za saratani lakini pia hukinga tumbo kupata vidonda vya tumbo kwa uwezo wa compounds mbalimbali ilizonazo. Compounds hizi zinazopatikana kwenye ndizi hujenga tabaka nene kwenye kuta za tumbo ambazo hukinga tumbo kuathirika na tindikali ijulikanayo kama ‘’hydrochloric acid’.

Pia ndizi zina enzyme inayojulikana kama ‘’protease inhibitor’’ ambayo huzuia bakteria wasababishao vidonda vya tumbo. Yani ukila ndizi tu unaweza usimwone daktari kwaajili ya tatizo la vidonda vya tumbo.

Kifua Kikuu – TB.

Ponda ponda ndizi mbivu moja kisha changanya na mtindi (curd) nusu kikombe, asali kijiko kidogo kimoja na maji ya nazi kikombe cha chai kimoja. Tumia mara mbili kwa siku kwa maana kwamba asubuhi utatumia ndizi moja na jioni ndizi ya pili.

Homa ya Tumbo – Typhoid.

Ponda ponda ndizi mbivu moja na changanya na asali kijiko kikubwa (table spoon) kimoja. Tumia mara mbili kwa siku kwa siku kadhaa hadi upone.

Tatizo la kuyeyusha Chakula – Indigestion.

Usiku wakati wa kulala kula ndizi mbivu moja na maziwa kikombe kimoja, mbali na matatizo yaliyoelezwa hapo juu, ndizi pia husaidia katika matatizo mengine mengi kama vile kutuliza mishipa ya fahamu, kuondoa wasiwasi, kushusha joto mwilini, kurekebisha mapigo ya moyo, n.k

Hivyo ndizi ni tiba ya magonjwa mengi na ni bora, ukiilinganisha na tofaha (Apple), ndizi ina protini mara nne zaidi, wanga mara mbili, vitamin A na chuma mara tano na vitamini na madini mengine mara mbili zaidi ya epo.

@Michael Sedekia.

Chama: Miquissone alitamani kurudi Simba SC
Nukuu tano za Jerry Silaa kuhusu sakata la Bandari