Serikali kupitia Wizara ya Afya, imejenga nyumba za Watumishi 52 zenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 3 katika Hospitali za Rufaa za Mikoa na Hospital za kanda, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuboresha utoaji huduma kwa wananchi.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel Bungeni Jijini Dodoma, wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu, Dkt. Ritta Enespher Kabati katika Mkutano wa kumi na moja na kuongeza kuwa nyumba hizo zimejengwa katika mwaka wa fedha 2022/2023. 

Amesema, “katika mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali imejenga nyumba 52 za watumishi zenye thamani ya shilingi bilioni 3,417,556,981 ikiwemo nyumba moja ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa na itaendelea kujenga nyumba kwaajili ya Watumishi na jambo hili litaongeza hamasa katika kuboresha utoaji huduma kwa wananchi.”

Aidha, Dkt Mollel ameongeza kuwa Serikali itaajiri Wataalamu wa afya, huku akisisitiza zoezi la kuhamisha Wataalamu hasa madaktari bingwa kulingana na mzigo wa wagonjwa wa kituo husika na kuendelea kuwaendeleza watumishi kupitia mafunzo ya ndani na nje ya nchi.

Mikoa ijipange udhibiti mambukizi ya Malaria - Majaliwa
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Aprili 26, 2023