Siku chache baada ya Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, kupiga marufuku taasisi na mashirika ya umma kutuma mizigo au vifurushi kwa kutumia Kampuni binafsi,badala yake zitumie Shirika la Posta Tanzania(TPC), imeanza kuzaa matunda baadhi ya taasisi hizo kuanza kuingia mkataba naTPC.

Hayo yamesemwa na Meneja wa Shirika la Posta Mkoa wa Mwanza, Julias Chifungo amesema zuio hilo limeanza kuwa na mafanikio kutokana na baadhi ya taasisi za umma kuanza kutumia TPC.

Aidha, amesema kuwa tangu Profesa Mbarawa atoe agizo hilo,TPC  Mkoa wa Mwanza imeweza kutembelea jumla ya mashirika na taasisi za Serikali zipatazo 1o2 ambapo kati ya hizo wameingia mkataba na mashirika 30 ambayo hadi sasa yameshaanza kutumia huduma zao.

”Zamani mashirika ya Serikali na kampuni binafsi yalikuwa yanafanya biashara huria,tunaushukuru uongozi wa awamu ya tano kwa jitihada zake za kuleta mabadiliko yenye tija ndani ya shirika letu la posta”amesema Chifungo.

Hata hivyo hayo yamekuja siku chache baada ya Waziri wa Ujenzi la kuzitaka taasisi na mashirika ya umma kuanza kulitumia shirika la Posta kwa kusafirishia mizigo.

Joe Biden amtaka Trump kujitambua
Jaffo aunda kamati ya uchunguzi hospitali ya Mkuranga