Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mchengerwa ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Zuberi Homela na viongozi mbalimbali wa CCM kwenye kijiji cha Mwanavala cha Wilayani Mbarali kutekeleza agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa la kufika kuona hali ya ugomvi wa mei 6, 2023 baina ya wananchi na wahifadhi na mifugo liyokamatwa na kuuawa, ambapo imethibitika kuwa hakuna kifo wala mifugo inayoshikiliwa au kuuawa.
Hoja hiyo, iliibuliwa na Mbunge wa Mbarali, Fransis Mtega aliyeomba kutoa hoja ya dharula ya kulitaka bunge lijadili suala hilo hatimaye Waziri Mkuu kutoa maelekezo hayo na ujumbe huo umewaona waathirika wa tukio hilo na viongozi mbalimbali wakafika eneo la tukio lenye kilomita 20 ndani ya Hifadhi kwa mipaka ya awali wa mita chache toka kingo za Mto Ruaha.
“Nimesikitishwa sana na kauli za Mbunge ambapo baadhi ya malalamiko na shutuma zake dhidi ya Serikali zimeleta taharuki kubwa ambayo sijaikuta katika eneo hili na kwamba wananchi wamekiri kuingia ndani ya eneo hili na wameiomba Serikali kuharakisha mchakato wa kuwatafutia maeneo ya kuishi.” amefafanua Mhe. Mchengerwa
Amezitaja baadhi ya tuhuma ambazo hazina ukweli na ambazo zimethibitishwa na wananchi wenyewe kuwa si kweli ni pamoja na wananchi kukataa kuwa hakuna mifugo iliyochukuliwa na wahifadhi 230 kama ilivyoripotiwa na Mbunge zaidi ya purukushani ya Mbwa wakali wa wananchi husika na wahifadhi, ambapo pia wananchi hao wamekiri kufanya shughuli zao ndani ya Hifadhi na wamewaomba kuzingatia sheria za uhifadhi.
Aidha, amewaonya viongozi wa kisiasa kuacha kuwachonganisha wananchi na serikali ambapo amesisitiza kuwa wananchi ni wahifadhi namba moja huku akimwelekeza Katibu Mkuu wa Maliasili kuchukua hatua dhidi ya askari waliohusika kuwachapa wananchi husika.