Watu kadhaa wanasadikika kujeruhiwa vibaya kwenye ajali ya gari iliyotokea mkoani Kilimanjaro ikihusisha roli na gari ndogo aina ya Noah ya abiria iliyokuwa ikifanya safari zake kati ya Sanya Juu – Moshi.

Ajali hiyo imetokea maeneo ya Kikavu karibu na Kwa sadala Mkoani Kilimanjaro ambapo Roli kubwa lilikuwa linajaribu kulipita gari lingine ndipo likakutana uso kwa uso na Gari ndogo aina ya Noah iliyokuwa imebeba abiria likitokea Moshi mjini kwenda Sanya Juu.

Aidha, taarifa kamili za ajali hiyo bado hazijatolewa na jeshi la polisi mkoani humo, lakini mashuhuda wa tukio wamsema kuwa huenda baadhi ya abiria waliokuwa kwenye Noah wamejeruhiwa vibaya.

Vile vile, wamesema kuwa watu wanne ndio wameonekana kupata majeraha makubwa na hali zao ni mbaya zaidi hivyo wamekimbizwa hospitali kwaajili ya matibabu.

 

Magazeti ya Tanzania leo Novemba 12, 2017
Trump, Putin kuliangamiza kundi la IS