Hospitali nchini Nepal imeanza zoezi la kuikabidhi miili ya watu 72 waliofariki katika ajali ya ndege iliyotokea Jumapili (Januari 15, 2022), wakati ikikaribia kutua mji wa Pokhara uliopo katikati mwa nchi hiyo ya Asia.
Wafanyakazi wa uokozi, wamekuwa wakifanya kazi bila kupumzika usiku na mchana, kuitafuta miili ya marehemu kutoka katika vipande vya ndege hiyo, ilioanguka kwenye korongo na kisha kuwaka moto.
Inaminika kuwa watu wote waliokuwa ndani ya ndege hiyo (wasafiri 68 na wafanyakazi wanne), walipoteza maisha.
Kwa mujibu wa maafisa wa Polisi nchini humo, wamesema Watoto sita na raia 15 wa kigeni ni miongoni mwa wahanga wa ajali hiyo na kwamba hadi kufikia mapema leo, miili 70 ilikuwa imepatikana.