Ali Kiba na Barakah Da Prince leo wamevamiwa na watu 6 wenye bunduki  jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini walipoenda kushoot video za nyimbo zao mpya.

Taarifa rasmi iliyotolewa na uongozi wa Rockstar4000 ambayo ndio inawasimamia wasanii hao imeeleza kuwa tukio hilo limetokea katika ofisi ya kampuni moja maarufu Afrika Kusini walipokuwa wakifanya mkutano na watayarishaji wa video wa kampuni hiyo.

“Wakati wakiendelea na mkutano, watu sita waliokuwa na bunduki walivunja kuta za jengo la ofisi hiyo na kuingia walipokuwa Alikiba, Barakah The Prince na wengine,” imeeleza taarifa hiyo.

Imeeleza kuwa watu hao wenye silaha walipora mali mbalimbali za wasanii hao na zilizokuwa kwenye ofisi hiyo na kutoweka nazo. Hata hivyo, watu hao wawakuwadhuru kwa namna yoyote wote waliokuwa ndani ya ofisi hiyo.

“Wote Alikiba na Barakah The Prince wanapenda kuwahakikisha mashabiki wao kuwa wako salama na wanapumzika kwa siku moja kusahau tukio hilo baya lakini wamenuia kuendelea na miradi yao na hawatazuia kutoa miradi yao ijayo iliyopangwa kwaajili ya mashabiki wao Afrika na duniani kote,” Rockstar4000 imeeleza.

Barakah Da Prince alijiunga na Rockstar4000 hivi karibuni na kuwa kwenye timu m0oja na wasanii walio chini ya kampuni hiyo, Ali Kiba na Lady Jay Dee.

Paper Towel Absorbency Lab Report
Lowassa awahakikishia Ukawa Ushindi 2020 kwa sharti moja