Msanii mkongwe wa nyimbo za bongofleva, Alikiba jana usiku ametangazwa rasmi kuwa mkurugenzi na sehemu ya wamiliki wa kampuni ya Rockstar4000 Music Entertainment and Rockstar Television inayojishughulisha na utengenezaji wa vipindi vya mastar tofauti kutoka nchi mbalimbali na kuvisambaza katika vituo vya Televisheni za kimataifa.

Hii ni baada ya msanii huyo kufanya kazi na kampuni ya Rockstar4000 kwa takribani miaka 6.

Alikiba sasa anakuwa sehemu ya wasanii waliochini ya Rockstar4000 pia anakuwa Mkurugenzi wa Vipaji na Muziki wa kampuni hiyo.

Jana jioni kupitia mtandao wa Instagram msani mkongwe wa nyimbo za bongo fleva, Alikiba aliwatangazia mashabiki wakae mkao wa kura kwani yupo mbioni kuwapa taarifa nyeti. Kupitia instagram aliandika hivi

”My Superfans! I will be making an exclusive announcement today with #RockstarTV – Register and Log on to https://www.younow.com/RockstarTV for the news and I will talk to all my fans LIVE by video stream! – Stand By for the Time will be announced soon…! Link on BIO wait for it
#kingkiba”

Chid Benz amkoromea Chin Bees, ampa onyo kali
Video: Pacquiao awageukia majaji , "nahisi nilifanyiwa njama"