Bondia mfilipino, Manny Pacquiao ambaye Jumapili iliyopita alipoteza pambano kati yake na bondia wa Australia, Jeff Horn amedai kufanyiwa mchezo mchafu ili apoteze pambano.

Pacquiao ambaye awali alieleza kuyaheshimu matokeo ya majaji na kumpongeza Horn, aliwaambia waandishi wa habari nchini kwake kuwa anahisi alifanyiwa njama na kwamba majaji na mwamuzi walikuwa na matatizo.

Horn alitangazwa mshindi wa pambano hilo katika matokeo yaliyozua utata, mbele ya umati wa zaidi ya watu 55,000.

Pacquiao alidai kuwa muamuzi wa pambano hilo hakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi kwa weledi na kwamba aliziangalia faulu nyingi dhidi yake bila kutoa onyo. Bondia huyo alipata mipasuko miwili kichwani na kifuani kutokana na kile kinachoaminika kuwa ni rafu alizokabiliana nazo.

“Sikutakata mwamuzi anipendelee mimi. Nilitaka uamuzi wake kwangu mimi na Horn uwe sawa. Kama nilipoteza nilipoteza, kama nilishinda nilishinda,” Pacquiao anakaririwa na ABS-CBN Tagalog.

Kadhalika, anadaiwa kueleza kuwa waamuzi wa pambano hilo hawakuwa na uhalisia na kwamba hata mtu anayeangalia video ya pambano hilo anaweza kusema alichokiona.

“Tuliongoza kwa raundi 4 au 5 dhidi yao, iko wazi hata ukiangalia mkanda wa pambano,” aliongoza.

Katika hatua nyingine, Pacquiao ambaye hakuhudhuria mkutano wa waandishi wa habari baada ya pambano alidai kuwa ametoa nafasi ya pambano la marudiano na kwamba atahakikisha timu yake inashiriki kikamilifu katika kuwaangalia waamuzi na majaji wa pambano watakaochaguliwa.

Alikiba atangazwa kuwa Mkurugenzi wa kampuni ya Rockstar4000
?LIVE: Rais Magufuli akizindua mradi wa maji Sengerema Mwanza