Mtu mmoha aliefukiwa na maporomoko ya mgodini kwa siku 3 huko Rongo nchini Kenya, amepatikana akiwa hai.

Mtu huyo kwa jina Noah Ogweno alizikwa siku tatu zilizopita ardhi ilipoporomoka akichimba migodi na amekuwa akitafutwa siku tatu tangu tukio hilo lilipotokea.

“Tunamshukuru Mungu kwa wema wake kulinda maisha ya Noah. Kikosi chetu cha uokoaji kimefaulu kumpata akiwa hai na kwa sasa anakimbizwa hospitali. Imekuwa ni masaa 72 tete wakati oparesheni hiyo ilikuwa ikiendelea. Ni maombi tu yamewezesha hili,” alisema Mbunge Abuor.

Familia yake imekuwa na kilio kwa siku tatu wakati ambapo shughuli za uokoaji zimekuwa zikiendelea.

Ripoti za kupatikana kwa Ogweno zilisisimua Wakenya na kumpa heko kwa kuvumilia masaa 72 akiwa ardhini.

Aidha wakati hili tukio likiendelea kisa kingine kimeendelea kushika kasi ambapo Tom Okwach alizikwa akiwa hai katika migodi mingine huku ikiwa ni siku 37 sasa tangu tukio hilo kutokea na familia yake haijapata usaidizi wa kumpata mpendwa wao.

Martin Sikuku, babake Okwach, alisema mwanawe alikuwa amepiga simu kabla ya Krisimasi ya 2021 akiahidi kuwa atawatumia pesa za kufurahia shamrashamra za Krisimasi.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Januari 12, 2022
Msukuma ataka kumrithi Ndugai