Katibu Mkuu  Ofisi ya Rais (Tamisemi), Jumanne Sagini jana alimsimamisha kazi aliyekuwa mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Mhandisi Mussa Natty ambaye hivi karibuni alipewa uhamisho wa kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati mkoani Manyara.

Akitoa sababu za uamuzi wa serikali kumsimamisha kazi Mhandisi Natty, Katibu Mkuu huyo alisema kuwa hatua hiyo imechukuliwa ili arudishwe katika Manispaa ya Kinondoni kusubiri uchunguzi wa tuhuma dhidi yake.

Alisema kuwa Mhandisi huyo anatuhumiwa kwa usimamizi mbovu wa wa barabara za Manispaa ya Kinondoni uliopelekea barabara hizo kujengwa chini ya kiwango huku akishindwa kuwawajibisha watumishi wa chini yake.

Sagini aliongeza kuwa Mhandisi Natty anakabiliwa na tuhuma za ukosefu wa uadilifu katika usimamizi wa ubinafsishaji wa eneo la ufukwe wa bahari wa Coco  pamoja na uratibu mbovu wa ugawaji wa viwanja katika manispaa hiyo.

 

Viongozi Wa Chelsea Wakutana Kumjadili Mourinho
Rais Magufuli Amuondoa Dk. Hoseah Takukuru, amteua huyu